Maswali ya Biblia kutoka Waraka wa Filemoni

 

S: Kwenye Flm, kitabu kifupi cha Filemoni kina thamani gani?

J: Kwa kuwa huu ni waraka kutoka kwa mtume Paulo, na ulipokelewa kama Maandiko Matakatifu na kanisa la kwanza, tunapaswa kukithamini cha Filemoni kama neno la Mungu, hata kama (tukizungumza kinadharia) tusingeona thamani yoyote ile ya Filemoni.

Hata hivyo, tunaweza kuona thamani kubwa ya kitabu hiki kidogo. Wakati vitabu vingi vingine vinajadili mafundisho na maisha, Filemoni , anatupa mfano mzuri wa moja ya njia ya kuhusiana na wakristo wenzetu katika masuala yenye utata.

Paulo anasema kuwa mtumwa huyu, ambaye hapo awali hakuwa na manufaa kwa Filemoni, amekuja kuwa na manufaa kwa Filemoni na Paulo. Sababu kuu ya mabadiliko haya kutoka kutokuwa na manufaa hadi kuwa na manufaa ilikuwa ni mabadiliko ya kiroho yaliyotokea wakati Onesimo alipompokea Yesu kama Mwokozi wa maisha yake. Kitabu cha Filemoni pia kinaonyesha kuwa ingawa Mungu alichukuliana na utumwa wakati ule, hayo hayakuwa mapenzi yake kamili.

Mwisho, waraka wa Filemoni unaweza kuitwa kitabu cha msamaha. Filemoni alipata hasara ya kifedha kwa kumwacha Onesimo huru, na Onesimo hakuwa amesamehewa kiasi, au kwa masharti, bali alisamehewa kikamilifu. Paulo alimsihi Filemoni amsamehe, lakini hakumlazimisha, kwa sababu msamaha unatakiwa uwe wa hiari.

 

S: Muhtasari wa Flm ni upi?

J: Hii hapa ni moja ya namna ya kukiangalia kitabu cha Filemoni:

Flm 1-3 Salamu kutoka kwa Paulo

Flm 4-7 Shukrani na maombi kwa ajili ya Filemoni

Flm 8-17 Ombi kwa ajili ya mtumwa aliyekimbia

Flm 18-22 Uhusiano wa Paulo na Onesimo

Flm 23-25 Salamu za mwisho na baraka

 

S: Kwenye Flm 1, ni kitu gani kisichokuwa cha kawaida kabisa kuhusu salamu ya Paulo hapa?

J: Kwenye barua zake nyingine Paulo amekuwa akitaja mamlaka yake, kama mtume, mtumwa wa Kristo, n.k., lakini Paulo hasemi lolote kati ya hayo kwenye barua yake hii kwa mtu mmoja, lakini kwa watu wengi kwa Filemoni. Badala yake Paulo anasema tu kuwa yeye ni mfungwa. Paulo anafahamu jinsi ilivyo kuwa chini ya mamlaka ya mtu mwingine.

Lakini Paulo ni mfungwa wa nani? Alifungwa baada ya kushtakiwa na viongozi wa Kiyahudi. Alipelekwa Rumi na askari wa Kirumi na kuwekwa katika gereza la Kirumi. Lakini Paulo haliangalii jambo hili namna hii. Badala yake Paulo anasema yeye ni mfungwa wa Kristo Yesu. Mwenye kuhusika na kumfunga, na kumfungua (au kutokumfungua), ni Kristo Yesu, na Yesu alikusudia Paulo kuteseka akiwa mfungwa kwa ushuhuda kwa watu wengine. Na Paulo anakubaliana na jambo hilo.

 

S: Kwenye Flm 1 na 2 Tim 1:8, Bwana alimchukuliaje Paulo kama mfungwa?

J: Paulo hakufungwa na Yesu; Paulo alifungwa kwa ajili ya Yesu, kama 2 Timotheo 1:12 inavyoonyesha. Warumi waliokuwa wanamlinda hakika wasingeliangalia jambo hili kwa namna hiyo. Hata hivyo, Paulo alikuwa na fursa ya kuchagua. Kwa kuwa Roho Mtakatifu alimwonya kuhusu kufungwa kwake kupitia nabii Agabo, Paulo angeweza kukimbia, bali alichagua njia hii kwa kukusudia kabisa akijua itamsababishia kufungwa.

 

S: Kwenye Flm 2, ni kitu gani kisichokuwa cha kawaida kuhusu jina Afia?

J: Katika utamaduni wa Kigiriki wa Kiionia wa eneo hili, Afia si jina lisilokuwa la Kigiriki, lililorekodiwa katika maandishi ya Kifrigia.

 

S: Kwenye Flm 4-5, kwa nini Paulo anamwandikia Philemoni kwa namna hii?

J: Paulo anamsifu Filemoni, si kwa upendo wake kwa watakatifu (waamini wa Kristo), bali kwa upendo wake kwa watakatifu wote, ambao Filemoni atakuja kulielewa kuwa kwa sasa anajumuishwa Onesimo. Filemoni alikuwa na sifa ya kuwa mwenye upendo na mcha Mungu, na Paulo anaanza kwa kumkumbusha jambo hili na kumsifu kwa ajili ya hilo, kisha anamwomba aionyeshe sifa yake hii kwa vitendo na kumfanyia Paulo fadhili.

 

S: Kwenye Flm 10, 2 Tim 1:2, Tit 1:4, na 1 Kor 4:17, kwa nini Paulo alimwita Onesimo, Timotheo, na Tito wanawe, kwa kuwa kwenye Mt 23:9 Yesu alikataza kumwita mtu yeyote baba?

J: Wafilipi 2:22 inaonyesha kuwa Paulo alimwita Timotheo mwanawe, si kwa sababu ya uhusiano wa kimwili, bali kwa kuwa Timotheo alikuwa karibu kama mwana kwenye kuhudumia ya injili.

Onesimo alikuwa na manufaa kama mwana, na mpendwa kama mwana wa Paulo, wakati Paulo alipokuwa Rumi.

Si uongo kutumia kielelezo ambacho si kweli kihalisia, kama mtu anayeongea na watu wanaomsikiliza wanajua kuwa ni kielelezo tu.

 

S: Kwenye Flm 10, je, kuna ushahidi wowote nje ya Biblia kuhusu Onesimo?

J: Unaweza kuwepo, kwa kweli. Andiko la Eusebius, Historia ya Kanisa 3:36, linataja barua ya Ignatius kwa Waefeso (sura ya 1). Ignatius anamtaja Onesimo kama mchungaji huko. Hata hivyo, hamuonyeshi wazi kabisa kuwa alikuwa ni Onesimo yule yule wa kwenye Agano Jipya.

 

S: Kwenye Flm 10-15, kwa nini Paulo anachukuliana na utumwa?

J: Paulo alizungumza kuhusu utumwa kwenye 1 Wakorintho 7:20-23. Paulo anamwambia Filemoni kwa njia isiyo ya moja kwa moja amwache huu Onesimo. Kuhusu sababu ya Paulo kutopinga utumwa, angalia maelezo kwenye Waefeso 6:5-8 na Waefeso 6:9.

 

S: Kwenye Flm 11, kwa nini Paulo anasema kuwa Onesimo hakuwa na manufaa hapo awali?

J: Kwa Kigiriki, jina Onesimo linamaanisha “muhimu” au “mwenye manufaa.” Paulo anacheza na maneno hapa, kwa kuwa Onesimo alikuwa mtumwa wa Filemoni aliyekimbia. Mtumwa anayekimbia hana manufaa sana.

 

S: Kwenye Flm 12, kwa nini Paulo ana imani na utii wa Philemoni, kwa kuwa Paulo hakuwa amemuagiza Filemoni kufanya kitu chochote kile?

J: Paulo alimwambia Filemoni kuwa ingawa alikuwa na haki kama mtume kumwamrisha, badala yake Paulo alikuwa anamhimiza tu Filemoni kumwacha huru Onesimo. Kwa hiyo Paulo alikuwa na imani na utii wa Philemoni kwa Mungu. Kama Filemoni alikuwa anatambua kuwa anapaswa kumpokea, kumsamehe, na kumwacha huru ndugu yake Mkristo, Paulo alikuwa na imani kuwa Filemoni Philemoni angefanya jambo linalompendeza Mungu. Yakobo 4:17 inasema, "Basi, yeye ajuaye kutenda mema, wala hayatendi, kwake huyo ni dhambi."

 

S: Kwenye Flm 12-15, Paulo anasema nini hasa?

J: Kuna mambo manne.

1. Paulo anamwomba Filemoni kitu ambacho atakielezea (Filemoni 8)

2. Onesimo awa mwana wa Paulo ki imani, amempokea Kristo (Filemoni 10)

3. Paulo amrudisha Onesimo kwa Filemoni (Filemoni 12)

4. Paulo anamwomba Filemoni amwache huru Onesimo, mtumwa wake aliyekuwa amekimbia ambaye Paulo alimrudisha kwa Filemoni.

Mara nyingi, tunamtumaini Kristo katika kufiksha ujumbe wa injili kwa mtu mwingine, lakini hatulazimiki kuamini kuwa mtu huyo amepokea Yesu. Tunafikisha ujumbe wa injili kwa namna nzuri  kadri tunavyoweza, kisha tunamtumaini Roho Mtakatifu kuleta matokeo, kwa kuwa hatujui kwa uhakika kama mtu anamfuata Kristo kweli au la. Lakini hapa Paulo alitakiwa aamini kuwa Filemoni alikuwa ameokolewa kweli, kwa jinsi atakavyomtendea Onesimo. Kuna nyakati ambazo tunahitaji kufahamu kwa uhakika kama mtu amempokea Yesu maishani mwake kweli au la. Tunaweza kuangalia matendo yao, lakini hatuwezi kujua mara zote nia nyuma ya matendo hayo. Tunatumainia kwamba tunapoamini, au kutokuamini, hatutakosea, lakini kama tutakosea, ni bora kukosea upande wa kutumaini kuliko upande wa kutia shaka.

 

 

S: Kwenye Flm 16, "katika mwili" inamaanisha nini?

J: Maneno haya yanaweza kuwa na maana tatu.

Rafiki: Maneno “katika mwili na katika Bwana” yanamaanisha kwamba Onesimo angemhudumia kimwili, na kumpa ushirika kama muumini. Hii huenda ikawa ndiyo sababu t maneno oleo la Biblia la NIV linayatafsiri maneno haya “kama mtu” (The Believer’s Bible Commentary uk.215). Toleo la Biblia la NET linasema, “naongea kama binadamu.”

Huenda akawa bado mtumwa: Maneno "katika mwili" yanahusu uhusiano binafsi kati ya mtu na mtu, lakini yanaweza pia kumaanisha kudumisha uhusiano wa bwana na mtumwa (The Bible Knowledge Commentary: New Testament, uk.773).

Ndugu wa kimwili: Filemoni na Onesimo walikuwa ndugu wa kimwili. Kwa maneno mengine, Filemoni alikuwa amemfanya ndugu yake mwenyewe kuwa mtumwa. Kitabu kit Wacha 1001 Bible Questions Answeredred, uk.314 kina maoni haya, lakini maoni haya hayaaminiwi  kwa kiasi  kikubwa.

Mtazamo wa pamoja katika tafsiri zote kuna mtazamo wa kurejesha uhusiano wa asili. Tafsiri ya Williams imeeleza kwa maneno yake yenyewe kwa  ufupi: "kama mtumishi na kama Mkristo."

 

S: Kwenye Flm 17, ni neno “mshirika” lina umuhimu gani hapa?

J: Neno hili halina maana ya mshirika kwa ujumla, bali bayana mshirika wa biashara, au mfanyakazi mwenzake.

 

S: Katika Phm 17-18, je, huu ni mfano wa fundisho la haki iliyotolewa kwa watu wasiostahili?

J: Kitabu kiitwacho 1001 Bible Questions Answered, uk.67-68 kinasema ndiyo. Kama ambavyo dhambi zetu zilivyohamishiwa kwenye "akaunti" ya Kristo, Paulo alijitoa kulipa kila kitu ambacho Onesimo alikuwa anadaiwa na Filemoni.

Kuna mambo matatu yanayofanana kati ya hili la Paulo kuchukua deni la Onesimo na upatanisho wa Kristo.

1. Si dhuluma kwa Paulo kulipa madeni ya Onesimo. Paulo alijitolea kumlipia kama ambavyo  Kristo alivyojitolea kwa ajili yetu.

2. Hakuna rekodi endapo Paulo alilipa deni hili, au Onesimo, au Filemoni alisamehe madeni yote. Vivyo hivyo, kafara ya Kristo ni kwa wote, lakini malipo hayafanyiki kwa watu wanaokataa kumkubali Kristo. Tofauti: Mifano mingi siyo mikamilifu, ikiwemo huu hapa. Ilikuwa ni uamuzi wa Filemoni endapo angekubali ombi la Paulo au la. Onesimo hakuwa na mengi ya kusema hapa. Kinyume chake, tunaokolewa kwa neema  "kwa njia ya imani", na kama Waebrania 4:2 inavyosema, ujumbe wa injili haukuwa na thamani kwa baadhi ya watu, kwa sababu haukwenda pamoja na imani.

 

S: Kwenye Flm 17-19, je Filemoni au wakristo wengine wasingehofia kuwa watumwa wao wangeweza kumuuliza Paulo ni wakati gani ambao wanaweza kwenda kwa Paulo? Kwa maneno mengine, vipi kuhusu "hatari” ya kuwahimiza watumwa wengine kukimbia, na mfano wa mabwana kutokuwaadhibu?

J: Inakadiriwa kwamba karibu nusu ya watu walioishi kwenye Himaya ya Rumi walikuwa watumwa. Hapo awali Warumi walichukuliana na uasi wa watumwa, na walitoa uzito mkubwa sana kwa watumwa wanaowakimbia mabwana wao. Hata hivyo, Filemoni hakupaswa kuwa na wasiwasi kuhusu "mteremko wa hatari"; hakupaswa kuhofia hatari hii; hakupaswa kufanya jambo baya kwa lengo la kuweka mfano wenye kuchanganya vichwa, nasi pia hatupaswi kufanya hivyo. Jambo hili lingetoa mfano, si kwa watumwa, bali kwa mabwana wakristo kuwa wapole kwa watumwa wao na tendo jema la kuwaacha huru.

 

S: Kwenye Flm 18, ni kanuni gani ya kitheolojia inayofundishwa hapa?

J: Hii ni kanuni ya matengenezo. Kama mtu aliibia kitu, au alifanya kosa, na amesamehewa, bado anapaswa kurudisha kitu alichokiiba. Kwa kiasi kinachowezekana, anapaswa kurekebisha kosa alilolifanya.

 

S: Kwenye Flm 19, mtu anapoteza kiasi gani kwa kumwacha mtumwa huru?

J: Kwa wakati ule, mtumwa mwanaume, kijana, mwenye afya, ambaye hajafunzwa aligharimu karibu dinari 500, na dinari ilikuwa ni mshahara wa siku moja wa mfanyakazi wa kawaida. Kwa maneno mengine, hii ni karibu mshahara wa mwaka mmoja na nusu. Lakini hatujui alikuwa mtumwa wa aina gani. Watumwa wengi walikuwa na ujuzi mkubwa, na walifanya kazi kama wahasibu, walimu, washauri, na maafisa wa serikali. Kwa hiyo, kuna uwezekano kuwa Onesimo alikuwa na thamani kubwa kuliko hiyo. Mwandishi wa Kirumi, Cicero kwenye Quincio Roscio Amerimo 28 anamtaja mtumwa mmoja, aliyenunuliwa kwa dinari 3,000, alikuwa amefunzwa na alikuwa baada ya hapo akawa na thamani ya dinari 50,000. Pia, hatujui kama Onesimo alimuobia Filemoni alipokimbia; alihitaji kupata hela ili asafiri kwenda Rumi kutoka mahali fulani.

 

S: Kwenye Flm 19, kwa nini Paulo anamkumbusha Filemoni kuwa anadaiwa na Paulo nafsi yake mwenyewe?

J: Kwa ajili ya Onesimo, Paulo anaendelea kuwa mkali hapa. Ujumbe hasa wa Paulo uko namna hii, "kama wewe, Filemoni, unanishukuru kwa kufikishia injili hata ili kuokoa nafsi yako, onyesha shukrani yako kwa kumwacha huru Onesimo kutoka katika utumwa.”

 

S: Kwenye Flm 19, je, haikuwa sahihi kwa Paulo kuongea kwa nguvu, uaminifu, na ujasiri kiasi hicho?

 

J: Hapana. Paulo aliwapenda Filemoni na Onesimo wote wawili. Paulo alijua kuwa kumwacha huru mtumwa kulikuwa kunagharimu kifedha, na ingawa kulikuwa kugumu, Filemoni alipaswa kufanya hivyo. Wakati mwingine wakristo wanapaswa kuwa jasiri kusimamia mambo mazuri, kwa ajili ya wengine.

 

S: Kwenye Flm 24 na Kol 4:14, kwa nini Paulo yuko pamoja na Dema, kwa kuwa Dema alimuacha kwa sababu aliupenda ulimwengu huu kwenye  2 Tim 4:10?

J: Kama watu wengine, mwanzoni Dema alimsaidia Paulo katika huduma kisha baadaye alimwacha. Je, Dema alirudi tena, na je Dema aliokoka? Tunaweza kutumaini hivyo, lakini hatuna rekodi yeyote kuwa hivyo ndivyo ilivyokuwa au la.

 

S: Kwenye Flm, je Filemoni alifanya jambo ambalo Paulo alimuomba?

J: Kitabu cha Filemoni hakisemi lolote kihusu jambo hili. Huenda jambo hili limeachwa wazi kwa sababu kutakuwa na nyakati katika maisha yetu ambapo, kama Filemoni, tutakuwa tunajua Mungu anataka tufanye kitu ambacho kinapingana moja kwa moja na utamaduni wetu au msukumo na makusudio yetu ya asili.

Kwa upande mwingine, Filemomi hakuichana barua (kwa kuwa ilihifadhiwa), hivyo hii ni ishara ya namna fulani kuwa alifanya jambo ambalo Paulo alimwomba.

 

S: Je, tunamfahamu mtu mwingine yeyote aliyeandika barua kwa niaba ya mtumwa aliyemkimbia bwana wake?

J: Ndiyo. Karibu miaka 60 baadaye, gavana wa kipagani Pliny mdogo alimwandikia barua Sabianus kwa niaba ya mtumwa aliyemkimnia Sabianus. The Expositor’s Bible Commentary juzuu ya 11, uk.456 inasema hivi.

 Mwandishi wa Kirumi Cicero anawataja watumwa watatu waliowakimbia mabwana wao kwenye maandiko yake. Mmoja alikuwa amefungwa gerezani. Nyakati nyingine walifunikwa macho na kulazimishwa kutembea kufuata mduara siku nzima kuendesha jiwe la kusagia, kama vile wanyama walivyokuwa wanafanya.

 

S: Flm iliandikwa lini?

J: Kwa kuwa iliandikwa wakati ambapo Paulo alikuwa mfungwa, na baada ya Paulo kutembelea eneo hilo, kuna nyakati mbili zenye uwezekano wa kuwa muda huo.

Mwaka 58-60 BK wakati Paulo alipokuwa mfungwa huko Rumi.

Mwaka 56 BK wakati Paulo alipokuwa amefungwa huko Efeso.

Wakati mwingine wenye uwezekano mdogo zaidi ni ule ambapo Paulo alikuwa amefungwa huko Kaisaria. Wasomi wenye kutilia shaka msomamo wa asili wa karne ya kumi na tisa wa shule ya Tubingen (Ujermani) kama vile F.C. Baur, walidai kuwa iliandikwa na mtu mwingine katika karne ya pili, lakini walijaribu kupinga uandishi uliotajwa wa karibu kila kitabu cha Agano Jipya, kwa hiyo si ajabu walipinga Paulo aliandila kitabu cha Filemoni pia.

Wakristo wengi wanaafikiana na muda wa baadaye, lakini Onesimo angeweza kukimbilia Efeso pia kama Rumi.

 

S: Ni mambo gani yanayofanana kwenye Flm na Kol?

J: Wasomi hawakubaliani kama vitabu hivi viwili viliandikwa wakati mmoja au miaka michache kati yao. Lakini kitabu kimoja kilikuwa barua kwa kanisa, na kingine barua kwa mtu binafsi na kwa kanisa (Phm 2). Kwa vyovyote vile, yafuatayo ni mambo yanayofanana.

1. Kolosai, pamoja na Hierapolis na Laodikia ilikuwa Frigia, na Afia lilikuwa jina la Kifrigia.

2. “Neema na amani kwako zitokazo kwa Mungu Baba yetu” Flm 3 na Kol 1:2b

3. Nyaraka zote hizi mbili zonaaminika kuwa ziliandikwa na Paulo na Timotheo, ingawa maudhui ya Filemoni bila shaka ni ya Paulo tu. Hata hivyo, inawezekana kuwa Timotheo alikuwa mwandishi wa Paulo.

4. Nyaraka zote mbili zinamhusu Arkipo (Kol 4:17; Flm 2)

5. “Imani yenu katika Kristo Yesu, na upendo mlio nao kwa watakatifu wote" (Kol 1:4) na "Upendo wako na imani uliyo nayo kwa Bwana Yesu na kwa watakatifu wote" (Flm 5)

6. "Salamu yangu mimi Paulo, kwa mkono wangu mwenyewe" (Kol 4:18a). "Mimi Paulo nimeandika kwa mkono wangu mwenyewe” (Flm 19).

7. Nyaraka hizi mbili zinamaliza kwa kusema, "Neema na iwe pamoja nanyi" (Kol 4:18b) na "Neema ya Bwana Yesu Kristo iwe pamoja na roho zenu" (Phm 25).

 

S: Kwenye Flm, kuna ushahidi gani wenye kuonyesha kwamba kitabu hiki kinapaswa kiwemo kwenye Biblia?

J: Kusema ukweli, kwa kuwa Filemoni ni kitabu kifupi sana, hakijanukuliwa sana na vitabu vingine. Zifuatazo ni sababu tatu tunazozijua kuwa kitabu hiki kinapaswa kuwa kweny Biblia.

1. Paulo alikiandika, na yeye alikuwa mtume. Mtume Petro alithibitisha kuwa maneno ya Mtume Paulo yalikuwa Maandiko Matakatifu kwenye 2 Petro 3:15-16.

2. Paulo mwenyewe alisema kuwa alikuwa mtume kwenye 1 Timotheo 1:1; 2:7, Warumi 1:1; 1 Wakorintho 1:1; 9:1, 2 Wakorintho 1:1, 11:5; Wagalatia 1:1, Waefeso 1:1; Wakolosai 1:1; 1 Timotheo 1:1; 2 Timotheo 1:1; Tito 1:1.

3. Ushahidi toka kanisa la mwanzo:

Muratorian Canon (mwaka 170-210 BK), ANF juzuu ya 5, uk.603 imasema kuwa Paulo aliyaandikia makanisa saba kwenye nyaraka zake: Wakorintho (barua 2), Waefeso, Wafilipi, Wakolosai, Wagalatia, Wathesalonike (barua 2), na Warumi. Paulo aliwaandikia Filemoni, Tito, na Timotheo (barua mbili).

Tertullian (mwaka 198-220 BK) anasema kuwa Marcion hakumwekea Filemomi "mikono ya uongo", ingawa hakutaja jina la kitabu hiki. Tertullian Against Marcion, kitabu cha 5, sura ya 21, uk.473 (ameongea si kwa wazi kabisa).

Origen (mwaka 225-253/254 BK) ananukuu Filemoni 14. "Paulo kwa ufahamu alimwambia Filemomi kwenye Waraka kwa Filemoni kuhusu Onesimo: Ili kwamba wema wako usiwe kwa kulazimishwa, bali kwa hiari" (Homilies on Jeremiah, Mahubiri ya 28, sura ya 2, uk.224.

Baada ya Baraza la Nikea

Eusebio wa Kaisaria (mwaka 326-339-340 BK) anawaongelea "wanajeshi wenzake" kama vile Filemoni 2 anavyofanya, lakini nukuu hii ndiyo ya karibu zaidi na Filemoni aliyonayo.

Hilary of Poitiers (mwaka 355-367/368 BK) ananukuu nusu ya kwanza ya Filemomo 1. "Soma Mitume: Paulo, mtumwa wa Kristo, anajivunia vifungo vyake. Hebu tuangalie endapo 'mfungwa huyu wa Yesu Kristo'" (On the Trinity, kitabu cha 4, sura ya 39, uk.83.

Athanasius of Alexandria (mwaka 367 BK) haongelei aya yeyote ile bayana ya Filemoni, bali anaorodhesha vitabu vya Agano Jipya kwenye Festal Letter  39, uk.552.

Synopsis Scripturae Sacrae (mwaka 350-370 BK au karne ya 5) inautaja waraka wa Paulo kwa Filemoni kama sehemu ya Agano Jipya. Inanukuu Filemoni 1 yote.

Cheltenham Canon (=Mommsen Catalogue) (karibu mwaka 360-370 BK).

Ephraim the Syrian (mwaka 350-378 BK).

Cyril of Jerusalem (karibu mwaka 348-386 BK) [Imeelezwa kwa namna isiyokuwa wazi].

Sinodo ya Laodikia - huko Frigia (mwaka 343-381 BK) canon 60, uk.159 inaorodhesha vitabu vya Agano la Kale na Agano Jipya. Canon 59, uk.158 inasema ni vitabu tu vilivyotambuliwa na kanisa vya Agano la Kale na Jipya vinaweza kusomwa kanisani. Ambrosiaster (baada ya mwala 384 BK) anataja Filemoni 2, 6, 12, 25.

Amphilochius  Iambi ad Selucum (mwaka 394 BK).

John Chrysostom (mwaka 396 BK) aliandika mahubiri matatu juu ya Philemoni. Anasema kuwa Paulo aliandika waraka huu kwa Filemoni, mtu mwenye kuvutia, kwenye mahubiri ya 1.

Syrian Catalogue of St. Catherine’s (karibu mwaka 400 BK) [Imeelezwa kwa namna isiyokuwa wazi].

Epiphanius Salamis (mwaka 360-403 BK) [Imeelezwa kwa namna isiyokuwa wazi].

Papa Innocent I wa Roma (karibu mwaka 405 BK)

Rufinus (mwaka 374-406 BK)

Baraza la Carthage - maaskofu 218 (mwaka 393-419 BK) [Imeelezwa kwa namna isiyokuwa wazi]

Jerome (mwaka 373-420 BK) aliongelea vitabu vya Agano Jipya. Anazungumzia bayana kila moja ya injili nne, nyaraka za Paulo kwa makanisa saba, Waebrania, nyaraka za Paulo kwa Timotheo, Tito, na Filemoni. Kisha Jerome kisha anaongelea Matendo ya Mitume. Baada ya hapo anaongelea nyaraka saba za Yakobo, Petro, Yohana, na Yuda. Mwishoni anaongelea Ufunuo wa Yohana. Barua ya 53, sura ya 9, uk.101-102.

Jerome (mwaka 373-420 BK) anaitaja Filemoni 2, 6, 12.

Augustino wa Hippo (mwaka 388-430 BK).

John Casian – baba wa Semi-Pelagianism (mwaka 419-430 BK).

Ushahidi wa wazushi na vitabu vya uongo.

Mzushi Marcion aliingiza Filemoni kwenye orodha yake ya vitabu vya Agano Jipya kwa mujibu wa Expositor’s Bible Commentary, juzuu ya 11, uk.453.

Mzushi Pelagius (mwaka 416-418 BK) anaongelea Filemoni 2, 6, 12.

Mzushi wa Upelegianism Theodore wa Mopsuestia (mwaka 392-423/429 BK) anaongelea Filemoni 6, 25.

Bado tuna ushahidi huu wote leo.

 

S: Tunajuaje kuwa Flm leo ni nakala ya kuaminika ya maandiko yaliyoandikwa awali?

J: Kuna sababu nzuri zisizopungua tatu:

1. Mungu ameahidi kuhifadhi neno lake kwenye Isaya 55:10-11; Isaya 59:21; Isaya 40:6-8; 1 Petro 1:24-25; na Mathayo 24:35.

2. Ushahidi wa kanisa la mwanzo. Angalia swali lililopita kuona baadhi ya waandishi walioongelea aya za Wafilipi. Hakuna yeyote aliyenukuu aya ya Filemoni.

3. Hati za mapema zaidi za Maandiko zilizopo za Philemoni zinaonyesha tofauti ndogo sana za maandishi kadhaa, bila ya kuwa na makosa ya kitheolojia.

p87 ina Flm 13-15, 24 (kwa sehemu), 25b na mapengo kadhaa (karibu mwaka 125 BK). Mwandiko unafanana sana na p46. The Complete Text of the Earliest New Testament Text  ina picha ya p87 kwenye ukurasa wa 607.

The Complete Text of the Earliest New Testament Text ina picha ya p87 kwenye ukurasa wa 608. Inasema kuwa wahariri wake wa kwanza walisema kuwa p87 iliandikwa “mapema karne ya tatu” kwa sababu mwandiko wake unafanana sana na p46, na p46 ilifikiriwa kuwa iliandikwa karne ya tatu. Kwa kuwa p46 inajulikana sasa kuwa iliandikwa mapema zaidi, inawekwa kuanzia katikati hadi mwishoni mwa karne ya 2. Ushahidi mwingine ni kuwa maandishi ya p46 na p87 yanafanana sana na Papyrus Oxyrhynchus 841 (iliyonakiriwa kwa mara ya pili mwaka 120-130 BK). Ushahidi wa tatu ni kuwa p87 inafanana kwa namna ya kushangaza na p52, ambayo inaaminika kuandikwa mwanzo wa karne ya pili.

p61 Warumi 16:23, 25-27; 1 Wakorintho 1:1-2, 2-6; 5:1-3, 5-6, 9-13; Wafilipi 3:5-9, 12-16, Wakolosai 1:3-7, 9-13, 1 Wathesalonike 1:2-3; Tito 3:1-5, 8-11, 14-15; Filemoni 4-7. Karibu mwaka 700 BK.

Karibu mwaka 700 BK-1968 – The Text of the New Testament.

Karibu mwaka 700 BK-1975 - Aland na wenzake toleo la tatu.

Karibu mwaka 700 BK-1998 - Aland na wenzake toleo la nne lililorekebishwa.

Sinaiticus [Si] mwaka 340-350 BK.

Filemoni haikuandikwa kwenye Vaticanus [B].

Alexandrinus [A] karibu mwaka 450 BK.

Bohairic Coptic [Boh] karne ya ¾ BK.

Sahidic Coptic [Sah] karne ya ¾ BK.

Ephraemi Rescriptus [C] karne ya 5 BK.

I Washington D.C. karne ya 5 (Flm 2, wengine?) Claromontanus [D] karne ya 5/6 BK.

The Text of the New Testament, uk.167, iliyoandikwa mwaka 1968, inasema kuna hati 10 za Maandiko yaliyoandikwa kwa herufi kubwa (pamoja na  wasahihishaji wanne) na hati 42 zilizoandikwa kwa herufi ndogo. Angalia www.BibleQuery.org/Philemon Manuscripts.html kwa maelezo zaidi kuhusu hati za mapema za Maandiko ya Filemoni.